loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Muuzaji bidhaa za asili atoa somo kwa jamii

MUUZAJI wa bidhaa za asili za kutunza ngozi, Eunice Panga anatoa wito kwa jamiii kutumia bidhaa za asili za kutunza ngozi badala ya zile zinazochubua.

Panga alitoa wito huo katika Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya Bidhaa yanayoendelea mkoani Dar es Salaam.


Panga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Paroti alijikita kwenye biashara hiyo ya kutunza ngozi mwaka jana baada ya kumaliza chuo lengo likiwa ni kuepusha matumizi ya bidhaa zenye kemikali ambazo zina athari kwenye mwili.
 

Alitaja bidhaa anazouza kuwa ni mafuta ya ubuyu, sabuni ya ubuyu, unga wa rosela pamoja na rose water kwa ajili ya kuipa ngozi unyevu.


Ameseema amekuwa akielimisha watu juu ya kutumia bidhaa asili kwa ajili ya kutunza ngozi na kutolea mfano wa mafuta ya ubuyu kuwa yana vitamin C na E hivyo yanasaidia kukinga ngozi na mionzi ya jua, kuondoa vipele na chunusi pamoja na ngozi kavu iliyokauka na kupasuka.

 

“Unga wa ubuyu una vitamin C nyingi zaidi ya machungwa pamoja na nyuzinyuzi zinazoongeza kinga mwilini, unga wa rosela pia unaongeza damu na vitamin C ambazo zinaongeza kinga ya mwili jambo linalotoa matokeo chanya katika ngozi,” amesema Panga.

 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Wanawake  Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mercy Silla amesema kuwa  maonyesho hayo ni ya siku 10 yaliyoanza  toka jumamosi iliyopita kuelekea siku ya wanawake duniani.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi