loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Diamond awapa somo wanawake

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Nassibu Abdul ‘Diamond Plutnumz’ amesema wanawake wanapaswa kuondoa dhana ya kuwezeshwa ndio waweze bali wapambane kutunza uanamke wao.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye uzinduzi wa wimbo mpya unaohusu wanawake wa Super Woman ulioimbwa kwa pamoja na wasanii mbalimbali akiwemo yeye kwa ajili ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, Diamond alisema mwanamke anaweza kuwa kiongozi, mwalimu au kufanya kazi yoyote iwapo akidhamiria kupambana.

Alisema kwake yeye anawaheshimu wanawake kwani wana mchango mkubwa katika maisha yake, huku akimtaja mwanamke shujaa kwake ni mama yake mzazi na mtoto wake wa kike Princess Tiffa.

“Mwanamke yeyote ni Super Woman, wana mchango mkubwa katika maisha, yeyote anayehangaika usiku na mchana kukomboa maisha yake hayuko katika kumtegemea mwanaume,” alisema.

Diamond alisema dhana ya mwanamke shujaa kwake ni yule anayepambana kuutunza uanamke wake na kufanikisha kila kitu. Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, Diamond ameungana na wasanii wengine zaidi ya wanane kutunga wimbo maalum wa Super Woma (Mwanamke shujaa).

Walioimba mbali na Diamond ni, Jux, Belle 9, Barnaba, Mbosso, Dulla Makabila, Lavalava, Joel Lwaga na G Nako.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi