loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yafia kwa Coastal

HATIMAYE zile tambo za mashabiki wa Yanga kwa timu yao kutopoteza mchezo kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana zilifi ka kikomo baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Coastal Union ya Tanga.

Matokeo hayo yameendelea kuipa wakati mgumu Yanga ambayo imekuwa na mwenendo wa kusuasua tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi, ambapo katika mechi nne walizocheza tangu kuanza mzunguko huo wamekusanya pointi nne.

Licha ya kuvunja rekodi ya Yanga kutopoteza mchezo tangu ligi ianze, Coastal Union, imeendeleza rekodi ya kutofungwa na klabu hiyo katika misimu mitano iliyopita, ambapo mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni misimu sita iliyopita kwa bao la Mganda Hamis Kiiza dakika ya 86.

Hata hivyo, pamoja na kipigo cha jana Yanga inaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya pointi 49 kwa michezo 22 iliyocheza, huku wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 45 na michezo mitatu mkononi.

Kwa mwenendo huo, Simba ambao pia ndio mabingwa watetezi wa taji hilo wana nafasi kubwa ya kuiengua Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi endapo itashinda mechi zao tatu za viporo zilizobaki.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani. Tanga, mabao ya Coastal Union yalifungwa na Erick Msagati dakika ya 10 na Mudathir Abdallah dakika ya 83 wakati bao la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 37.

Mapema dakika ya sita, Kisinda alipoteza mkwaju wa penalti baada ya mlinzi wa Coastal Union kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji wa Yanga Fiston Abdulrazak, baada ya tukio hilo Coastal walifanya shambulizi la kustukiza na kupata bao la kwanza.

Kisinda alisawazisha makosa yake dakika ya 37 baada ya kufunga kwa kichwa mpira ambao alitanguliziwa na Yacouba Sogne aliyeingia muda mchache kuchukua nafasi ya Michael Sarpong ambaye katika mchezo huo alionekana kutokuwa

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Mohammed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi