loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Papa Francis kuanza ziara ya kihistoria Iraq

PAPA Francis ameanza ziara yake ya  kwanza rasmi nchini Iraq na safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu kuzuka kwa ugonjwa wa  corona.

Safari hiyo ya siku nne aliyoianza jana inakusudiwa kuihakikishia ushirikiano jamii ya Kikristo inayopungua ya Iraq na kukuza mazungumzo ya dini.

Papa atakutana na kiongozi wa Waislamu wa dhehebu la Kishia anayeheshimiwa sana, na kufanya sala huko Mosul na kuhudhuria misa katika uwanja wa michezo.

Kiongozi huyo alisisitiza kufanya ziara hiyo licha ya ongezeko jipya la maambukizi ya covid-19 nchini Iraq na hofu dhidi ya usalama wake.

Saa kadhaa baada ya shambulio la roketi dhidi ya kambi ya wanajeshi wa Marekani siku ya Ijumaa, Papa alisema Wakristo wa Iraq hawawezi kuvunjwa moyo kwa mara ya pili.

Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Papa Francis ya kimataifa kuifanya tangu janga la covid-19 lilipoanza, mwaka juzi.

Papa John Paul wa Pili alifuta mpango wa safari nchini humo mwishoni mwa mwaka 1999 baada ya mazungumzo kati yake na Rais wa Iraq wakati huo Saddam Hussein kuvunjika.

Ndani ya miongo miwili tangu wakati huo, moja ya jamii ya zamani ya Wakristo duniani imeshuhudia idadi yake ikipungua kutoka milioni 1.4 hadi karibu 250,000.

Baadhi yao wamekimbilia ughaibuni kwa kuhofia mashambulio kwa misingi ya kidini ambayo yamekumba nchi hiyo tangu Marekani ilipoivamia kijeshi mwaka 2003 na kumuondoa madarakani Saddam.

Maelfu ya watu pia wamekimbia makazi yao baada ya wanamgambo wa Islamic State (IS) kuteka eneo la kaskazini mwa Iraq mwaka 2014, na kuharibu makanisa ya kihistoria, kuchukua mali zao na kuwapa masharti ya kuachana na dini yao ama wauawe.

Mkuu wa Kanisa Katoliki la Roma analenga kuwatia moyo Wakristo wanaoteswa na kushinikiza amani katika mikutano na viongozi wa kisiasa na kidini.

Akiwahutubia watu wa Iraq kupitia ujumbe wa video mkesha wa safari yake, Papa Francis alisema anaenda nchini humo kama hujaji, msafiri anayetubu, kumuomba Mungu msamaha na upatanisho baada ya miaka kadhaa ya vita na ugaidi, kuomba faraja kutoka kwa Mungu na uponyaji wa mioyo wa majeraha.

" Nakuja miongoni mwenu pia kama hujaji wa amani…kutafuta ushirika unaotokana na hamu ya kuomba pamoja na kutembea pamoja, pia na ndugu na dada zetu wa dini nyingine katika nyayo za Baba Abrahamu , ambaye anajiunga na familia moja ya Waislamu ,Wayahudi na Wakristo,” alisema.

Papa aliiambia jamii ya Wakristo wa Iraq kuwa anataka kuwaletea upendo mzuri wa Kanisa lote ambalo liko karibu nao na eneo la Mashariki ya kati lillokumbwa na vita, kuhimiza maendeleo mbele kwa imani.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani , viongozi wa Kikristo wanakadiria kuwa kuna Wakristo wachache kuliko 250,000 waliosalia Iraq.

MAREKANI imejiunga kwenye mazungumzo yanayolenga ...

foto
Mwandishi: ROME, Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi