loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mke wa mwanamfalme ashutumu kasri kwa kuendeleza uongo dhidi yake

MKE wa mwanamfalme  Harry,Meghan Markle amesema kwamba Kasri la Buckingham haliwezi kutarajia yeye na mumewe ( Harry)  kunyamaza iwapo linaendelea kusambaza madai ya uongo dhidi yake.

Meghan aliyasema hayo katika kanda moja ya mahojiano katika kipindi chake na Oprah Winfrey.

Meghan alikuwa ameulizwa alihisi vipi kuhusu kasri hilo kumsikia akisema ukweli na kueleza kuwa endapo kusema kwake ukweli kutakuja na hatari ya kupoteza vitu na kusema tayari kuna vitu vimeshapotea.

Kasri la Buckingham linachunguza madai kwamba wawili hao walimnyanyasa mfanyakazi wa ufalme huo. Madai ya unyanyasaji yaliyowasilishwa dhidi ya Meghan yalichapishwa baada ya mahojiano na Winfrey kurekodiwa.

Mahojiano hayo na Winfrey ambayo yatapeperushwa moja kwa moja siku kesho nchini Marekani keshokutwa nchini Uingereza, yanatarajiwa kuelezea utendakazi wa Harry na Meghan katika kipindi chao kifupi wakiwa wafanyakazi wa ufalme kabla ya kujiuzulu ili kwenda kuishi Marekani.

Katika kanda ya pili ya sauti iliyotolewa na CBS, Winfrey anawauliza wanawafalme hao : Je munahisi vipi kasri la Buckingham likisikia mkizungumza ukweli hii leo?.

“Sijui jinsi walivyotarajia kwamba baada ya muda huo wote tungebakia kimya, iwapo kuna mpango wa kasri hilo kusambaza uwongo kutuhusu sisi,” alisema.

Wawili hao walijiondoa katika kazi zao kama wafalme Machi, mwaka jana na sasa wanaishi California.

Ripoti moja katika gazeti la Times katikati ya wiki hii lilidai kwamba mke huyo wa mfalme alilalamikiwa kufanya unyanyasaji wakati alipokuwa akifanya kazi ya ufalme huo.

Barua pepe iliyovuja iliyotumwa na mfanyakazi mmoja, ambayo ilichapishwa na gazeti hilo, inadai kwamba Meghan aliwaondoa wasaidizi wawili kutoka katika jumba hilo.

Taarifa katika gazeti hilo la Times pia iliongezea kwamba alimkandamiza na kumuondolea kujiamini mfanyakazi wa tatu wa ufalme huo.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Meghan akijibu gazeti hilo ilisema: Mwanamfalme huyo amesikitishwa na shambulio dhidi ya tabia yake hususani kama mtu ambaye amekuwa akilengwa na kwamba amekuwa akiwaunga wale ambao wamekuwa wakinyanyaswa.

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: CALIFORNIA Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi