loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gekul audhiwa na waliovamia shamba  la chanjo

NAIBU  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul amewataka viongozi waliohusika kuuza eneo la shamba la Taasisi ya Chanjo (TVI) Kibaha wachukuliwe hatua za kisheria  na wananchi waache kundelea kuuziana sehemu hiyo hadi pale Wizara ya Ardhi itakapotoa tamko juu ya watu waliovamia shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 1,037  .

Gekul aliyasema hayo mjini Kibaha alipotembelea kituo hicho ambacho zamani lilikuwa shamba la kuzalishia ng’ombe wa kisasa (mitamba) kuwa viongozi hao wameendelea kuwauzia watu eneo hilo mali ya serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

 “Hapa hili ni kama jicho letu kwani tuna malengo 13 ya kipaumbele mojawapo ni kuzalisha chanjo hivyo wenyeviti na mabalozi waliohusika wachukuliwe hatua kwani, ” alisema Gekul.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Martin Ntemo alisema kuwa walitoa maelekezo kwa wavamizi hao kuondoka na kwa wale waliojenga wabomoe wenyewe kabla serikali haijachukua hatua ya kubomoa na wasiendeleze chochote kutokana uvamizi mkubwa uliofanyika.

Meneja wa kituo cha chanjo Kibaha, Dk Stella Bitanyi alisema kuwa shamba hilo lilikuwa kubwa likamegwa Halmashauri wakakabidhiwa baada ya tathmini wakaambiwa waendeleze hekta 2,963 na wao wakabakiwa na hekta 1,037 lakini bado wananchi waliendelea kulivamia ndipo walipoanza utaratibu wa kuomba namna ya kusaidia kurejesha eneo hilo ambapo watu wa awali ni wawili tu walilipwa fidia lakini wavamizi wameongezeka na kufikia mamia ya watu.

Bitanyi alisema kuwa wananchi wengi walijitokeza wakiwa na hati kabla ya kituo hicho hakijapima na wizara ya ardhi ilipopima wakajua kuwa ndiyo wataruhusiwa kukaa hapo lakini walipoona kimya wakaendelea kuvamia wakidai eneo ni lao ambapo uvamizi huo unaendelea hadi sasa.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi