loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyakazi wapya Kilimo wapigwa msasa

JUMLA  ya watumishi 36 wa Wizara ya Kilimo Makao Makuu juzi wameanza kupata mafunzo yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusu maadili ya utumishi wa umma pamoja na utoaji wa huduma kwa umma.

Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili kwa niaba ya Katibu Mkuu,  Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu ,Philbert Lutale alisema mafunzo hayo ambayo wizara imeyatoa kwa watumishi wapya yanalengo la kuwaandaa watumishi hao kwenda sambamba na mahitaji ya nyakati pamoja na mahitaji ya wateja.

Kaimu Mkurugenzi Lutale aliongeza kuwa utoaji wa huduma kwa wananchi walio kwenye Sekta ya Kilimo Mazao unaongozwa na Dira ya Wizara inayosema, “ Wizara itakuwa kiini cha kutoa mwongozo wa sera na huduma kwa kilimo cha kisasa na chenye tija faida na ushindani kibiashara ili kuimarisha ustawi wa Wananchi, usalama wa chakula na lishe.” hivyo wizara inawatarajia baada ya mafunzo hayo watakuwa mahili kwenye maeneo ya maadili ya utumishi wa umma, Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma,  utunzaji wa kumbukumbu na taratibu za ofisi.

Margaret Ngondya kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuandaa mafunzo hayo kwa watumishi wake.

Margaret aliongeza kuwa katika siku hizo mbili watumishi wa wizara watajifunza kuhusu misingi ya maadili katika utumishi wa umma na kanuni zake nane ambazo ni kutoa huduma bora, utii kwa serikali, bidii ya kazi, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu,  kuwajibika kwa umma, kuheshimu sheria na matumizi sahihi ya taarifa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi