loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Alat Tanga wachaguana

MWENYEKITI  wa Halmashauri ya Korogwe vijijini Sadick Kallaghe amefanikiwa kuibuka mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) Mkoa wa Tanga kwa kupata kura 17 huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na Mstahiki Meya wa jiji la Tanga, Abdulrahman Shiloo aliyeshinda kwa kura 32 kati ya kura 40 zilizopigwa.

Akizungumza mara baada ya kuibuka na ushindi katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Alat mkoa wa Tanga, Kallaghe aliahidi kuhakikisha analeta sura mpya katika chombo hicho cha mkoani Tanga kwa kuibua kitega uchumi kitakachowezesha kuwaingizia mapato mkoani humo.

Katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Alat mkoa ilikuwa ikishindaniwa na watu watatu akiwemo Sadick Kalaghe aliyepata kura 17, Erasto Mhina kutoka wilayani Muheza aliyepata kura 10  na  Idrisa Mgaza kutoka wilayani Kilindi akipata kura 13.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa  mwenyekiti Alat Mkoa ilikuwa ikishindaniwa na watu wawili akiwemo mstahiki meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo aliyepata kura 32 na  Mussa Mkombati akipata kura nane.

Awali akizungumza katika kikao hicho Kallaghe aliwashukuru wajumbe wa Alat mkoani Tanga kwa kumpa heshima na nafasi hiyo na kuahidi kuwa mbunifu kayika kuibua miradi mbalimbali itakayowawezesha kuwaingizia kipato.

Alisema atahakikisha anashirikiana na madiwani wa kata zote 245 za Mkoa wa Tanga kwa kuhakikisha wanapata maslahi yao stahiki kwa kushirikiana na serikali kuu.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti Alat Mkoa Tanga Abdulrahman Shiloo alisema atahakikisha anashirikiana na mwenyekiti kwa kufanya kazi pamoja ili kutimiza, malengo ya Alat waliojiwekea.

foto
Mwandishi: Amina Omari, Lushoto

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi