loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kila la kheri Simba

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba leo wako ugenini Khartoum, Sudan kumenyana na Al Mirrikh ya huko.

Tayari Simba ilishafika Khartoum tangu juzi na kusifia aina ya mapokezi waliyopata na kudai hawatakuwa na kisingizuo chochote zaidi ya kucheza mpira kutafuta ushindi.

Kwa nyakati tofauti kocha wa Simba Didier Gomes amesema mechi hiyo itakuwa ngumu sababu wapinzani wao wameshapoteza mechi mbili tayari hivyo mechi hii ya mwisho ya mzunguko wa kwanza kwenye kundi lao watajitahidi kushinda na hapo ndipo ugumu unapotokea.

Tunamuunga mkono Gomes kwamba haitakuwa mechi rahisi kwa hakika hivyo hana budi yeye kama mkuu wa benchi la ufundi kuongeza mbinu za ushindi.

Wachezaji pia bila shaka wanafahamu umuhimu wa kushinda mechi hiyo kwa hiyo wamejiandaa kupata matokeo mazuri katika mechi hiyo.

Simba inatakiwa kufahamu kuwa inawakilisha taifa hivyo watanzania wote wapo nyuma yao kwasababu watakapofanya vizuri faida itapata nchi.

Tunaamini mipango yote iko sawa huko Khartoum na kama ilivyo matarajio ya wengi basi leo wawakilishi hao wataibuka na ushindi katika mechi hiyo.

La muhimu ni kwa wachezaji kufuata maelekezo yote waliyofundishwa na benchi lao la ufundi na wasitishwe na hujuma zozote zitakazotokea wakati ama kabla ya mchezo huo kwani hayo ndio mambo ya mchezo huo Afrika.

Tunaamini kama ni hujuma, fitna kwa wachezaji zimeshazoeleka sasa, hivyo watafanya vizuri.

Kila lenye Kheri Simba.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi