loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkongo wa Taifa kufika kila wilaya, kata nchini

WIZARA ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  imesema kuwa inatarajia kufikisha Mkongo wa Taifa kila wilaya na kata, kurahisisha mawasiliano kwa wananchi, ambapo kwa sasa imefikia wilaya 24 kwa urefu wa kilometa 68,000.

Naibu Waziri, Andrea Kundo alitoa mwito huo jana alipofanya ziara  katika wilaya ya Kibaha  Mkoa wa Pwani, ambako alikutana na watoa huduma za mawasiliano.

Kundo alisema kuwa lengo ni kufika wilaya zote nchini na matarajio ni kufika kwenye kata ili kuweza kutoa njia rahisi ya kubeba masuala ya mawasiliano kwa wananchi na kuboresha huduma ya biashara mtandao.

"Baada ya hapo tunatarajia kufikia ofisi za viongozi ili Watanzania wawe na matumizi ya data kwa urahisi ili kuleta tija kwa nchi katika masuala ya mawasiliano katika kujiletea maendeleo kupitia njia ya mawasiliano,"alisema Kundo.

Alisema katika kuhakikisha wananchi hasa walio pembezoni, wanapata huduma ya mawasiliano, serikali ilianzisha Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote mwaka 2006.

"Mfuko huu unatoa ruzuku kwa makampuni ya mawasiliano ili wasaidiwe kujenga minara kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara ili Watanzania waweze kupata huduma ya mawasiliano ambapo hadi sasa umefikisha mawasiliano kwenye kata 1,057 ,"alisema Kundo.

Alisema mfumo wa huduma mawasiliano kwa wote, unaangalia kwenye shule na kwamba katika halmashauri 185 nchini, unalenga kuhakikisha angalau shule mbili  zinapata kompyuta tano na printa moja.

“Pia upande wa wanawake, watoto wa kike na Tehama miundombinu na vifaa hivyo pia hutolewa kwa watu wenye ulemavu, afya unafanya pale ambako wengine hawapaoni,"alisema Kundo.

Aliongeza kuwa changamoto ya mawasiliano maeneo ya Kibaha kama vile Pangani, Dutumi na Viziwaziwa, serikali imeandaa mpango wa tathmini nchi nzima, kujua wapi kuna tatizo wakati mwingine idadi ya ongezeko la watu ambapo watoa huduma wanaweza kuongeza uwezo na mifumo iliyokuwa imejengwa nyuma.

Meneja wa Kampuni ya Siku ya TTCL Mkoa wa Pwani, Jane Mwakalebela alisema kuwa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu.

Aliomba serikali kuwawezesha kujenga ofisi ambazo zitakuwa za kisasa kuendana na wakati, ambapo itakuwa ni njia mojawapo ya kuwavutia wateja kwa kuwa na mazingira mazuri kwenye ofisi hizo ambazo ni za muda mrefu.    

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo alisema kuwa suala la mawasiliano hasa vijijini na maeneo ya pembezoni mwa miji bado kuna tatizo kubwa, ambapo baadhi ya sehemu mawasiliano ya simu hakuna na kuwafanya wananchi kupata huduma kwa kiwango cha chini.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi