loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SIMBA QUEENS YAISHUSHA YANGA PRINCESS

TIMU ya Soka ya Yanga Princess imetolewa katika uongozi wa ligi na watani wao wa jadi Simba Queens baada ya kula kichapo cha mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya wanawake kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana.

Mabao ya bSimba yalifungwa na Mwanahamis Omari dakika ya 29, Opa Clement dakika ya 42 na Joelle Bukuru dakika ya 49.

Ushindi huo unaifanya Simba Queens kupanda juu ya msimamo kwa kufikisha pointi 39 katika michezo 15 Yanga ikishuka na pointi zake 38 wote wakiwa wamecheza michezo 15.

Hii ni mara ya kwanza Yanga inapoteza mchezo tangu kuanza kwa ligi ya wanawake msimu huu.

Awali, wenyeji Yanga walianza kwa kasi mpira kama dakika mbili za mwanzo kwa kuingia langoni kwa wapinzani wao kisha wakaanza kupoteza mwelekeo baada ya Simba kutulia na kucheza mpira wa pasi na kumiliki mpira hadi kupata bao la uongozi.

Kitendo cha wekundu hao kucheza kwa utulivu mkubwa na kujiamini huku wakifanya mashambulizi mengi kiliwafanya watani zao kushuka na kurudi nyuma kulinda lango hatua iliyowafanya kupoteza kujiamini kwa kuwa walikuwa wanapoteza mipira.

Dakika ya 41 mchezaji wa Yanga Princess Happiness Mwaipaja alioneshwa kadi nyekundu baada ya kudaka mpira akiwa katika jukumu la kuokoa mashambulizi ya Simba waliovamia lango lao wakati kipa Husna Zuberi akiwa ameanguka chini.

Kadi hiyo ni kama iliwafanya watani zao kukubali kipigo na kuamua kucheza kulinda lango lao na mashambulizi yao yakiwa machache.

Simba Queens ilitawala mpira vipindi vyote viwili na wangeweza kuondoka na ushindi zaidi ya huo kutokana na nafasi walizotengeneza

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi