loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara wanawake waunganishwa

CHAMA cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), kimewakutanisha wanawake wafanyabiashara kwa lengo la kuwaunganisha na soko pamoja na kujifunza kutoka kwa wengine jinsi ya kuandaa bidhaa zao hadi kufika sokoni.

Mwenyekiti wa TWCC, Mercy Silla alisema hayo katika Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonesho ya Bidhaa yanayoisha leo katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Silla alisema kusanyiko hilo ni fursa kubwa kwa wanawake hao wafanyabiashara kwani wametoka katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema chama hicho kimefarijika na maonyesho hayo kwa kuwa muitikio wa wafanyabishara umekuwa ni mkubwa japo kuna changamoto zilizojitokeza ambazo watazifanyia kazi.

“Tumekuwa tukipokea mapendekezo mbalimbali ya jinsi ya kuboresha maonyesho haya kwa msimu mwingine, tutayafanyia kazi lengo likiwa kila mmoja aweze kufaidika nayo pamoja na kutanua mtandao wake ikiwa na kuuza bidhaa anazozitengeneza, “ alisema.

Alisema miongoni mwa mambo ya kuyaboresha ni eneo la kufanyia maonyesho hayo, kutoa ushauri kwa wanawake hao kutokuwa na bidhaa zinazofanana ikiwa ni pamoja na kuwa na vitu tofauti tofauti vinavyovutia.

Alisema maonyesho hayo ni fursa kwani yamewaunganisha wajasiriamali hao kwa mfanyabiashara mmoja anaweza kuwa na bidhaa ambayo ni malighafi kwa mwingine ama mwingine anapopata oda kubwa anashirikiana na mwenzake katika kuikamilisha.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi