loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kujenga mradi wa maji Chamwino

Mbunge wa Chamwino Jijini Dodoma, Deo Dejembi amesema kuwa Serikali ipo katika mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi milioni 500 katika Kata ya Dabalo wilayani Chamwino.
 

Dejembi  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma amebainisha hayo leo jimboni humo alipokuwa ziarani  kutembelea wapiga kura wake.  
 
“Serikali ndani ya miezi mitatu baada ya kufuatilia imekubali kuleta mradi mkubwa wa maji hapa Dabalo ili kumtua Mama Ndoo na utakuwa msaada pia kwa maeneo jirani ya Segala na Membe” amesema Dejembi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi