loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wabadhilifu wa dawa na tiba kufungwa Jela

 

NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Godwin Mollel amewaonya watu wote wenye tabia ya ubadhilifu wa dawa na Tiba kuwa watafungwa kutokana na tabia hiyo.

Rai hiyo aliitoa wakati wa ziara yake mkoani hapa. Dk Mollel alisema ubadhilifu hautakiwa na watu watafungwa.

‘’Lengo la Serikali ni kuhakikisha ubadhilifu wa dawa unaondoka. Watu wote watakaofanya ubadhilifu wa dawa/Tiba tutawafunga na kuwapeleka Magereza’’ alisema Dk Mollel.

Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachunzibwa alisema Serikali imetoa msaada wa vitanda 50 katika hospitali ya Buchosa wilayani Sengerema.

Alisema katika mwaka huu wa fedha 2020/2021 Serikali imewatengea milioni 500 kwajili ya vifaa Tiba katika hospitali hiyo.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Mwanza,Jarlath Mshashu alisema mfuko wao utaendelea kusaidia Sekta isiyokuwa rasmi kupitia vifurushi vya Inajali,Inatimiza na Wekeza.

Alisema pia wanavyo vifurushi vya watoto ambayo inaitwa Toto Afya kadi inayohusisa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0-18. Alisema katika Halmashauri za Buchosa,Misungwi na Sengerema wamekuja na kifurushi cha Ushirika Afya ambapo kifurushi hiki kinahudumia wakulima wa mazao ya Kahawa na Pamba.

Mshahu alisema mpaka sasa kwenye kifurushi hicho wamejiunga wakulima 850 na tayari wakulima hao wamepata bima zao za  Afya.

 

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi