loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndumbaro awapa kipaumbele wasafiri wa anga na meli

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amesema kuwa wadau wa usafiri wa anga na meli ni watu muhimu sana katika sekta ya utalii kwakuwa wageni wengi  wanaokuja nchini kutoka nje hutumia vyombo hivyo.
 

Ndumbaro amebainisha hayo leo mkoani Morogoro wakati akifungua Mkutano wa Wadau wanaojihusisha na utoaji wa Huduma za Usafiri wa Anga na Meli. 

“Sekta hii ni muhimu sana kwakuwa hakuna mtalii anayetoka nje ya nchi anayefika hapa bila uwepo wenu  ndio maana mimi nipo hapa kama kiashiria cha kutambua mchango mnaotoa katika sekta ya utalii” amesema Ndumbaro.

Aidha, Ndumbaro amesema kuwa mkutano huo ni fursa nzuri kwa Wizara kutambua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wadau hao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kitu kitakachopelekea sekta ya utalii kupiga hatua kubwa.

 

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Ndege Tanzania (TAOA), Lathifa Sykes amesema kuwa ndege kubwa kutoka mataifa mbalimbali duniani haziwezi kupeleka watalii katika maeneo ya hifadhi hivyo wanapofika nchini jukumu hilo ulifanya wao.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi