loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Aweso awakalia kooni wakandarasi wabovu

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amepiga marufuku wakandarasi wasio na uwezo kupewa kazi ya usimamizi na ujenzi wa miradi ya maji nchini, kwani wamekuwa ndio chanzo cha miradi mibovu.

Alito agizo hilo wakati akifungua kikao cha wadau wa sekta ya maji mkoani Tanga kilichofanyika wilayani Lushoto.

Aliongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha kero kwa wananchi na kwa serikali, kwani inakuwa tayari imeshatumia fedha lakini miradi haijakamilika.

Alitaka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA), kuacha kutoa kazi za ujenzi wa miradi kwa wakandarasi wasio na uwezo na sifa ili Watanzania waweze kupata huduma kwa wakati.

“Kazi ya kutoa kandarasi za ujenzi wa miradi kwa wakandarasi wasio na uwezo ifike mwisho kwani najua mnawajua walio na uwezo na wasio na uwezo, sitaki ushangazi na ujomba kwenye utekelezaji wa miradi ya maji kwa sasa,” alisema Waziri Aweso.

Alisema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha maeneo ya vijijini upatikanaji wa huduma za maji unafikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025. Aliitaka RUWASA kupunguza michakato isiyo ya lazima katika ujenzi wa miradi hiyo.

Waziri Uweso alisema kuwa Rais John Magufuli amekuwa akitoa fedha kila mwezi, kuhakikisha wananchi wa vijiji wanapata huduma hiyo kwa haraka na hivyo kuwaondolea kero ya kutembea mwendo mrefu kufuata huduma hiyo.

Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikishs ifikapo mwaka 2025 kiwango cha upatikanaji wa huduma za maji kiwe kimeongezeka na kufikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini.

Aliwataka watendaji katika sekta hiyo, kusimamia kwa ukaribu utekekezaji wa miradi ya maji ili iweze kuwa endekevu na ya kudumu.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alisema kuwa mwaka jana pekee serikali ilipeleka  Sh bilioni  12 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Alisema kuwa kukamilika kwa baadhi ya miradi katika maeneo ya vijijini, kumeongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma hiyo hadi kufikia asilimia 70 kwa sasa.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Upendo Lugongo alisema  kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatatua kero ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya vijijini.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Amina Omari, Lushoto

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi