loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara sajilini biashara -TPSF

MWENYEKITI wa Taasisi za Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Anjelina Ngalula amewataka wafanyabiashara kusajili biashara zao ili waingie katika mfumo rasmi unaotambulika kisheria.

Ngalula alisema hayo kwenye Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonesho ya Bidhaa yanayoendelea katika viwanja vya Posta, Kijitonyama Dar es Salaam yanayomalizika Jumapili.

Alisema Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), ipo kwa ajili ya kuwahudumia wafanyabiashara na ni taasisi ya serikali ambayo imeboresha huduma zake, kwa kuwa mtu anaweza kujisajili kupitia mtandao na kupata cheti chake kwa haraka, tofauti na zamani.

“Tunawaomba wafanyabiashara wale wanaotaka kusajili biashara zao wahakikishe wanakuwa na zile nyaraka muhimu zinazotakiwa ili iwe rahisi kwao kujisajili.  Nasema hivyo kwa sababu kumekuwa na malalamiko kwa watu kuwa kuna changamoto katika kujisajili, lakini kumbe inatokana na nyaraka zinazohitajika kutojitosheleza," alisema.

Aliwapongeza BRELA kwa kuwepo katika shughuli yao hiyo ya sekta binafsi ya wanawake kwa sababu inaonesha ni jinsi gani ilivyo karibu na wafanyabiashara.

“Tayari wanawake wameiitikia na kusajili biashara zao, hiki ndicho kitu tunachokipigania kila mara, watu watoke kwenye mfumo usio rasmi waje kwenye mfumo rasmi, watoke huko ambako hawatambuliki ambapo huwezi kupata mkopo kama hujajisajili na biashara yako haijulikani," alisema.

Alisema kujitokeza kwa wingi kwa wafanyabiashara kwenye maonesho hayo kujisajili na wakala huo, ni hatua kubwa katika biashara zao.

Ofisa Leseni wa Brela, Sweetnes Madata alisema huduma wanazozitoa ni kusajili biashara, makampuni na alama za biashara, wanatoa leseni za biashara na leseni za viwanda.

Alisema ili mfanyabiashara asajiliwe anapaswa kuwa na nyaraka muhimu ikiwemo namba ya kitambulisha cha Taifa (NIDA), uthibitisho wa eneo analokaa na taarifa za biashara yake.

Madata alisema wapo kwenye maonesho hayo ili kuwa karibu na wajasiriamali na wawasaidie kurasimisha biashara zao, zitambulike kisheria pamoja na kuwapa ushauri wa jinsi ya kurasimisha biashara zikiwa zimetambulika na faida zake

Alisema tangu maonesho hayo yalipoanza, wamerasimisha biashara nyingi na wanaaendelea mpaka mwisho.

Mfanyabiashara, Marcelina Biro alisema amefika katika viwanja hivyo na kufanikiwa kusajili biashara yake kwa muda mfupi kisha kuondoka na cheti.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi