loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakazi Dar, Moro wahimizwa kutembelea vivutio Kisarawe

WAKALA wa Misitu Tanzania (TFS) umewaomba wananchi hususani wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na mingine  ya jirani, kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko wilayani Kisarawe mkoani Pwani ikiwamo Msitu wa Kazimzumbwi wenye vivutio vya kipekee.

Mhifadhi Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Fredy Ndandika alisema hayo katika banda la taasisi hiyo, inayoshiriki Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani, juzi.

Alisema moja ya maeneo yanayostahili kutembelewa na wanachi na wakafurahia ni Msitu wa Kazimzumbwi.

“Msitu huu wa asili wa Kazimzumbwi unapatikana Kisarawe na una vivutio vingi ikiwamo hali ya utulivu ambayo humpendeza kila mmoja anayeutembelea,”  alisema Ndandika.

Mbali na utulivu, ndani ya msitu huo kuna njia za watembea kwa miguu, mapango ya popo na mapango ya mizimu ambayo jamii ya Wazaramo huyatumia kwa ajili ya matambiko na kuomba.

Ndandika alisema kivutio kingine kinachopatikana katika wilaya ya Kisarawe na ambacho anashauri wananchi wajitokeze kutemblea ni Bwawa la Minaki, ambalo hutumika kwa ajili ya utalii wa uvuvi na kupiga picha.

Vivutio vingine ni maeneo ya kupumzikia yenye sifa ya kuwa na hewa safi na pia maeneo ambayo yanamwezesha mtu kusimama na kuona kwa uzuri mandhari ya jiji la Dar es saalam.

Alisema Msitu wa Kazimzumbwi ndio pekee unaotegemewa kwa kunyonya hewa chafu inayozalishwa Dar es Salaam na maeneo ya jirani na Kisarawe.

“Tupo kwenye tamasha la utalii la Kisarawe Ushoroba Festival ambapo lengo kuu la tamasha hili ni kutangaza utalii na vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya wilaya ya Kisarawe na kuonyesha fursa za uwekezaji katika wilaya yetu.

"Katika wilaya ya Kisarawe kuna utalii wa aina mbili, utalii wa kiutamaduni na utalii wa kiikolojia. Huu  wa Ikolojia unapatikana katika Hifadhi ya Mwalimu Nyerere ambayo sifa yake ya pekee ni kuwa hifadhi kubwa zaidi nchini," aliongeza Ndandika

Alisema TFS ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia Hfadhi ya Mwalimu Nyerere na watatumia vyema siku tatu za Tamasha la Kisarawe Ushoroba, kutangaza fursa zilizopo ili kuvutia watalii na wawekezaji.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo, Mkuu wa Walaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo alisema wameamua kuchochea juhudi za kutangaza utalii wilayani mwake ili kutengeneza fursa za ajira na kuwezesha wananchi wengi, kuona vivutio mbalimbali viliyoko Kisarawe.

Jokate aliwapongeza TFS kwa kushiriki tangu mwanzo wa majadiliano kuhusu kufanikisha tamasha hilo. Alisema anawatambua TFS kuwa ni wadau wakubwa pamoja na wadau wengine.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi