loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waalimu 30 Taekwondo wanolewa  Arusha 

Waalimu 30 Taekwondo wanolewa  Arusha 

JUMLA ya walimu 30 wa mchezo wa Taekwondo wanashiriki  semina maalumu inayofanyika katika ukumbi wa Njiro Complex,  mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la Taekwondo Tanzania (TFF) Richard Kitolo alisema semina hiyo inahusisha waalimu wa mchezo huo kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Alisema semina hiyo ni kwa ajili ya kuwapa ujuzi na kuwaongezea uelewa wa kuijua Taekwondo kiundani ili wanapofundisha waweze kuendana na sheria zake.

Semina hiyo inaendeshwa kwa nadharia na vitendo na wakufunzi David Samson kutoka Arusha na Majaliwa Patrick kutoka Dar es Salaam.

Akifungua semina hiyo Ofisa michezo mkoa wa Arusha,  Mwanvita Okeng'o  aliwaaasa walimu waende kutumia utaalamu watakaoupata katika shule za msingi na sekondari ili kusaidia  kukuza mchezo huo hapa nchini.

Alisema mkakati wa  serikali ni kuzalisha wataalamu wa kutosha katika kila mchezo na kusema semina zinazoandaliwa zinasaidia kujenga zaidi .

"Shirikisho la Taekwondo liandae mashindano mbalimbali kuanzia ngazi za mikoa na taifa ili kusaidia walimu kujitathimini kutokana na mafunzo wanayoyapata na wote waendelee kuzingatia miiko ya mchezo huo kwa kuwa na nidhamu,"alisema Okeng'o.

Naye mkufunzi David Samson alisema lengo la semina hiyo ni kufundisha walimu wawe na weledi zaidi kwa kufuata sheria na mtaala wa dunia wa Taekwondo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/60beaf6477a1ea99cf8ae840c11f6960.png

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi