loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mapato yaongezeka Bandari ya Kigoma

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Deusidedit Kakoko amesema kuwa Bandari ya Kigoma imeanza kutoa matokeo chanya kwa kuongezeka idadi ya  shehena za mizigo pamoja na mapato baada ya kufanyiwa maboresho makubwa.  


Kakoko amebainisha hayo mkoani humo alipotembelea bandari hiyo na kuongeza kuwa mapato yake yameongezeka kuipita Bandari ya Mwanza iliyokuwa ikiongoza mara baada ya kuboreshwa.  


“Bandari ya Kigoma inahusisha bandari zote zilizopo  katika Ziwa Tanganyika na ilianza kufanyiwa marekebisho toka mwaka 2016 katika maeneo yake mbalimbali na kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kabla ya kukamilika kwake lakini tayari imeanza kutoa matokeo chanya” amesema Kakoko.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi