loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wamiliki wa hoteli za kitalii waombwa kuboresha huduma 

SERIKALI imehimiza wawekezaji zaidi katika  ujenzi wa  hoteli za  kitalii  na  zilizopo, ziboreshe huduma zake  kwa gharama nafuu, kila Mtanzania aweze kutalii katika   hifadhi mbalimbali za taifa nchini. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro alitoa mwito huo juzi wakati akifunga mkutano wa siku nne mjini Morogoro wa  wadau wa utalii  kwa ajili ya kujadili kuhusu kuongeza idadi ya watalii na mapato, yatokanayo na shughuli za utalii nchini.

Dk Ndumbaro alisema ingawa zipo hoteli za kutosha katika hifadhi  mbalimbali nchini , serikali inaendelea kukaribisha uwekezaji zaidi katika sekta ya hoteli  kwa ajili ya kutosheleza malazi ya idadi yoyote ya watalii .

"Ukitembelea mbuga za taifa unaweza kulala hoteli ya dola 9,000 kwa siku moja na pia unaweza kulala hoteli kwa shilingi 30,000, huo ni uwezo wa mtu mwenyewe  tu ulale wapi , kwa hiyo hoteli zipo nyingi  za viwango tofauti ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata stahiki yake,” alisema.

 

Waziri Ndumbaro alirejelea hotuba ya Rais John  Magufuli ya ufunguzi wa  Bunge la 12,  Novemba 13,  2020  iliyosisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya utalii nchini ili iweze kuchangia zaidi katika pato la taifa.

Alisema masuala hayo pia yamesisitizwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, hususan katika ibara ya 67.

Alisema kuwa utalii ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi, ambayo inachangia zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yote ya nje na asilimia 60 ya mapato yote yatokanayo na biashara za huduma.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi