loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Ishengoma, Dk Kilonzo waula Na Rahel Pallangyo

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amesema wamefanya uteuzi wa watendaji muhimu katika sekta ya sanaa nchini.

Akizungumza Dodoma jana, Dk Abbasi alisema walioteuliwa ni Dk Emmanuel Ishengoma kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika wizara hiyo.

“Kabla ya uteuzi huo Dk Ishengoma alikuwa Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Haki na Maendeleo ya Wasanii na alikuwa pia akikaimu nafasi aliyothibitishwa sasa,” alisema Dk Abbasi.

Pia, alisema Dk Kiagho Kilonzo ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB).

“Kabla ya uteuzi huo Dk Kilonzo alikuwa anakaimu nafasi hiyo katika Bodi ya Filamu akitokea wizarani,” alisema Dk Abbasi.

Aidha, alisema uteuzi wa viongozi hao umeanza rasmi Machi 1, na wadau wa tasnia ya sanaa wanaombwa kuwapa ushirikiano wakati huu serikali ikiendelea kufanya mageuzi katika sekta hiyo muhimu nchini.

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi