loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Mwinyi atoa maagizo Manispaa ya Mjini

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameuagiza uongozi wa  Manispaa ya Mjini kuhakikisha walengwa pekee ndio wanapatiwa maeneo ya kufanyia biashara  katika  soko la muda lililojengwa eneo la Kibandamaiti. 

Dk Mwinyi ameto agizo hilo leo Jumamosi katika hafla ya kupokea soko hilo la muda na kubainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza vurugu kwa siku za baadae.

“Wafanyabiashara wanaopaswa kupewa nafasi katika soko hili ni wale waliokuwa wanafanya biashara zao katika Soko la Kijangwani na maeneo mengine yaliyokuwa siyo rasmi, hivyo nasisitiza kuwekwa utaratibu mzuri katika ugawaji maeneo ya kufanyia biashara” amesema Dk Mwinyi.

Soko hilo la muda limejengwa na vikosi vya ulinzi na usalama na hadi kukamilika kwake limegharimu kiasi cha shilingi milioni 6.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi