loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Taasisi kujenga viwanja vya michezo Ilemela

TAASISI ya Sports Charity imeahidi kuhakikisha inajenga viwanja 10 vya michezo katika wilaya ya Ilemela.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa vya michezo kwa timu za Ilemela,Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rogasian Kaijage alisema mpaka sasa tayari wamejenga viwanja vya michezo katika kata ya Mirongo pamoja na kata ya Sabasaba.

Alisema katika wilaya ya Ilemela watajenga viwanja vya michezo mbali mbali kumi.

‘’Tunaomba sana wakurugenzi watusaidia katika kutupa maeneo sisi tutajenga viwanja kwa gharama zetu.’’ alisema Kaijage.

Kaijage pia alisema Taasisi yao itaendelea kutoa vifaa vya michezo. Amewaomba viongozi wa Serikali kuwasidia katika kuwasamehe kodi ili waweze kuleta vifaa vingine zaidi vya michezo kwa timu mbali mbali za mkoa wa Mwanza.

Alisema watatoa mipira 10 kwa timu 50 za wilaya ya Ilemela.

Alisema michezo nchini inakabiliwa sana na tatizo la miundo mbinu jambo ambalo linakwamisha kuweza kuendelea kwa michezo.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela,Angelina Mabula amesishukuru taasisi hiyo kwa juhudi zao za kuendeleza michezo wilayani Ilemela.

Alisema Ilemela imekuwa ikifanya kazi na Halmashauri hiyo tokea mwaka 2015 na taasisi hiyo imekuwa ikiwasaidia kuwapa vifaa vya michezo wa mpira wa miguu,kikapu,netiboli na mpira wa wavu.

Amevitaka vilabu kuhakikisha vinatumia vyema mipira iliyopewa ili kuleta matokeo chanya katika michezo.

Kocha kutoka timu ya Jonas FC,Abdallah Maruzuk alisema anaishukuru Taasisi hiyo kwa vifaa walivyowapa.

Ameomba wadau wengi waendelee kujitoa na kuzisaidia timu za Ilemela ili ziwe kufanya vyema katika ligi mbali mbali.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga,Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi