loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maboresho Haki za Watoto kutumia bilioni 47

MPANGO Mkakati wa Pili wa Maboresho Endelevu ya Haki za Mtoto Nchini utakaotekelezwa kwa miaka mitano kati ya 2020/21-2024/25 unakisiwa kugharimu Sh bilioni 49.6 hadi kukamilika kwake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome alisema  pamoja na mambo mengine umelenga kuenzi na kuendeleza yaliyoanzishwa katika Mpango Mkakati wa Kwanza wa 2013-2017.

Profesa Mchome alisema Mpango Mkakati wa Pili unalenga kuendelea kuboresha mambo yanayoleta tija kwenye utoaji wa haki kwa mtoto nchini yaliyoanzishwa katika mpango wa kwanza, yakiwemo ya uanzishwaji miundimbinu ya ulinzi wa mtoto kwenye vyombo vya dola na vile vya utoaji haki.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi