loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake Viongozi watakiwa kuwasaidia wenzao

OFISA Mtendaji Mkuu wa Shirika linalokuza upatikanaji wa haki nchini Tanzania (LSF), Lulu Ng’wanakilala, amewataka wanawake waliopo kwenye uongozi kuzitumia nafasi hizo kuwasaidia na kuwainua wanawake wenzao.

Akizungumza katika mahojiano kwa njia ya simu, Lulu alisema anaitazama  kama siku muhimu kwa  mwanamke duniani akiwa kiongozi wa taasisi inayopigania haki za wanawake.

Kaulimbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu inasema ‘Mwanamke katika Uongozi, Chachu Kufikia Dunia yenye  Usawa,’.

Lulu alisema wanawake waliopo kwenye nafasi za uongozi wanapaswa kuwa mfano na chachu ya kuhamasisha wanawake wengine waweze kufikia kwenye nafasi hizo na pia wazitumie   kutumia nafasi za uongozi walizonazo kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla.

“Kwa hiyo kwangu mimi siku ya wanawake duniani ni muhimu katika kutambua usawa na haki za wanawake kwa ujumla, kutambua nafasi ya mwanamke kwenye jamii, kwenye familia, kwenye ngazi zote, haki ya mwanamke ya kutowekwa kwenye mazingira ya kupoteza haki zake ikiwemo ukatili wa kijinsia na haki ya mwanamke katika maamuzi,”alisema Lulu.

Alisema kwa muda mrefu haki za wanawake zimekuwa zikikosekana, hivyo siku ya wanawake duniani pia ni ya kukumbushana kuhusu umuhimu wa haki za wanawake, usawa na nafasi ya mwanamke katika jamii

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi