loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Papa Francis aongoza Ibada Iraq

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameongoza ibada katika Kanisa Katoliki la Walkadea la Mtakatifu Joseph mjin Baghdad, Iraq.

Papa Francis anakuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kuongoza misa kwa kutumia Liturujia ya Ibada ya Kanisa Katoliki la Mashariki. Papa mwenye umri wa miaka 84 amewambia waumini wa kanisa hilo kuwa sio matajiri na wenye nguvu ambao wamebarikiwa bali wale wanaowahurumia ndugu zao.

Mkuu wa Kanisa Katoliki la Waldaea, Kadinali Louis Raphael Sako, amesema ziara ya Papa Francis imepokelewa kwa furaha na kanisa lote.

Aidha, Papa Francis ambaye yupo ziarani nchini Iraq, alishiriki pia mkutano wa kihistoria  na kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, Ayatollah  al –Sistani kwenye mji mtakatifu wa Najaf. Pia alizuru eneo linaloaminika kuwa sehemu aliyozaliwa Baba wa Imani Abraham

MAREKANI imejiunga kwenye mazungumzo yanayolenga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi