loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madaktari Wakatoliki Kenya waikataa chanjo ya corona

MADAKTARI Wakatoliki nchini Kenya wamepinga kutolewa chanjo kukabili virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19. Taarifa ya Chama Cha Madaktari Wakatoliki Kenya (KCDA) ilieleza kwamba, hakuna haja kwa Wakenya kutumia chanjo hiyo kwa kuwa si muhimu.

Madaktari hao walitoa mwito kwa taasisi za kidini kutotumia chanjo hiyo kwa kuwa njia pekee iliyothibitishwa kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo ni kuvaa barakoa, kuwatenga waathirika wenye dalili, kutibu wagonjwa na kuhakikisha wagonjwa wote wa COVID-19 kuwa kwenye uangalizi kwa siku 10 hadi 14.

Katika taarifa hiyo, Dk Stephen Karanja alitoa mwito kwa Wakenya wasitumie chanjo na kwa ujumla isitolewe kabisa. Alhamisi iliyopita Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alizindua ugawaji wa chanjo ya corona akibainisha kwa, watumishi wa sekta ya afya na wanaohudumia wagonjwa wa COVID-19 wangekuwa wa kwanza kupata chanjo hiyo.

Chanjo Kenya ilitarajiwa kuanza kutolewa Ijumaa iliyopita na pia ilitarajiwa kuanza kutolewa siku hiyo nchini Rwanda. Mwezi uliopita Uswis ilikataa kuithibitisha chanjo ya Oxford AstraZeneca.

Hivi karibuni Afrika Kusini ilisitisha mpango wa kutaka kuwachanja wananchi wake chanjo aina ya Oxford-AstraZeneca kwa madai kuwa matokeo ya chanjo hiyo ni ya kukatisha tamaa. Wanasayansi nchini humo walisema maambukizi mapya ya virusi vya corona yalifikia asilimia 90 nchini humo.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Zweli Mkhize, alisema serikali itahitaji ushauri wa kitaalamu wa ama kuendelea na chanjo hiyo au la baada ya kuonesha matokeo hafifu na yasiyotarajiwa.

Afrika Kusini ilipokea dozi milioni moja za chanjo ya AstraZeneca na ilikuwa inatarajia kuanza kuwachanja watu wiki ijayo. Mkhize alisema chanjo ya AstraZeneca haioneshi matokeo mazuri kwa wagonjwa wenye dalili za kawaida na za kadiri, hivyo serikali itatoa chanjo zilizotengenezwa na kampuni za Johnson & Johnson na Pfizer.

Alisema utafiti uliofanyika kuhusu chanjo hiyo uliowahusisha watu 2,000, na kwamba, utafiti haujaweza kuchunguza ufanisi wa chanjo katika kuzuia maambukizi makali kwa kuwa washiriki walikuwa na umri wa wastani wa miaka 31 sampuli ambayo haiakisi kundi la watu wanaoweza kuwa na hatari ya kuugua zaidi wanapopatwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Hapa Tanzania Rais John Magufuli alishaweka msimamo wa kutopokea chanjo yoyote ya Covid-19. Wakati akizindua shamba la miti Chato mkoani Geita mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Magufuli aliwataka Watanzania kuwa waangalifu na chanjo hizo.

“Mtatishwa sana ndugu zangu Watanzania, lakini simameni imara. Najua wapo baadhi ya Watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine kwenda kuchanjwa, na walipochanjwa huko wametuletea corona ambayo ni ya ajabu ajabu, simameni imara, chanjo hazifai,”alisema.

Alisema kama chanjo za Covid-19 zingekuwa za kweli hata chanjo ya Ukimwi, kifua kikuu, malaria na saratani nazo zingekuwa zimeshapatikana, hivyo Watanzania hawana budi kuwa waangalifu na wasidhani wanapendwa sana.

Rais Magufuli alisema, si kila chanjo ni ya maana kwa taifa hivyo aliitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto isiwe inakimbilia chanjo bila kujiridhisha.

“Ni lazima Watanzania tuwe macho, ni lazima Watanzania tuwe waangalifu, tutafanyiwa majaribio ya ajabu ambayo yataleta madhara makubwa. Ninaomba tuendelee kusimama na kumuomba Mungu wetu”alisem

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi