loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maandalizi sensa ya watu na makazi yapamba moto

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanza mchakamchaka wa kufanya maandalizi ya sensa ya watu na makazi yakiwemo ya kutenga maeneo na kuandaa ramani za maeneo zitakazotumika. Sensa hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Agosti 2022.

Katika kufanya maandalizi ya sensa hiyo na ili kufanikisha suala hilo la kitaifa, NBS wiki iliyopita ilitangaza nafasi 300 za kazi za muda za kutenga maeneo mbalimbali katika mikoa yote 26 nchini Tanzania Bara.

Akizungumza na HabariLeo, Kaimu Meneja wa Idara ya Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Benedict Mugambi amesema maandalizi yanaendelea vizuri kwa kutenga maeneo madogo madogo na kuandaa ramani.

Alisema sensa ina hatua tatu, hatua ya kwanza ndiyo hiyo ya kutenga na kuandaa ramani; Hatua ya pili ni sensa yenyewe na hatua ya tatu ni kufanya tathmini baada ya sensa.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Sylvia Meku wakati akizungumza na Baraza la Wafanyakazi wa ofisi alisema ofisi hiyo inadhamana ya kufanya sensa na hivyo wanatakiwa kujiandaa na kujipanga kuhakikisha wanafanikisha.

Meku alisema kutokana na kuwa nyuma ya muda wawakilishi wa wafanyakazi wa ofisi hiyo waliopo katika nchi nzima, wanatakiwa kuanza kukimbia katika kufanya maandalizi ya sensa hiyo ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10 , mara ya mwisho ilifanyika 2012.

Alisema kutokana na kuthamini suala la sensa, Serikali tayari imetekeleza ahadi yake ya kutoa fedha kwa ajili ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi. Meku pia aliagiza Kurugenzi husika kukaa na wadau wa sensa kwa ajili ya kupitia na kuboresha mpango kazi na mkakati wa Sensa ya Watu na Makazi ili uendane na muda na mahitaji ya sasa.

Aidha, aliagiza Kurugenzi inayoandaa Sensa kuwashirikisha kikamilifu watumishi wa idara zote za NBS

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi