loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtendaji UCSAF ataka wanawake wasisahau familia

OFISA Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amewataka wanawake viongozi kutosahau majukumu yao ya kifamilia wanapoonesha ushupavu wa uongozi kwenye maeneo ya kazi.

Pia ametoa rai kwa Wanawake kutoshiriki vitendo vya ukatili kwa watoto na kusisitiza haja ya kusimamia malezi bora yatakayojenga maisha yao. Mashiba alitoa rai hiyo jana wakati wanawake wa mfuko huo wakitoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 4.5 kwa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini jijini hapa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani leo.

Mashiba alisema wanawake hasa viongozi wanapaswa kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa uadilifu na ufanisi mkubwa huku wakiendelea kutambua kuwa wao ni wazazi na walezi wa familia.

Alisema ili taifa liendelee kuwa na watoto waliolelewa katika misingi bora ya kifamilia, wanawake hasa viongozi wanatakiwa kutambua kuwa nafasi za uongozi walizonazo si mbadala wa majukumu yao katika familia.

“Nitoe wito kwa wanawake wenzangu hasa viongozi unapokuwa katika majukumu ya kikazi onyesha ushupavu wako, lakini unaporudi nyumbani usiwe kiongozi wa baba timiza majukumu yako kama mwanamke, wewe ni mama, tusilisahau hilo,”alisema.

Aidha, Mashiba alisema baadhi ya familia zimekuwa kwenye migogoro ambayo inasababisha unyanyasaji na kutengana kwa wazazi hali ambayo inachangia ongezeko la watoto yatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Akizungumzia hatua ya kuadhimisha Siku ya Wanawake, Mashiba alisema wameamua kutoa mchango huo kama taasisi kwa ajili ya kuchangia huduma mbalimbali zinazotelewa katika kituo.

Aidha, Mashiba aliwataka wana jamii wote kuwa na desturi ya kutembelea vituo mbalimbali kwa ajili ya kuwafariji watoto hao ikiwemo na kuwasaidia kuwapatia mahitaji mbalimbali kadri wawezavyo

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi