loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

China yataka mahusiano mazuri na Marekani

SERIKALI ya China imesema inatarajia Marekani itabadili sera za serikali iliyopita na kufanya uhusiano wa China na Marekani kurudi katika njia nzuri kwa manufaa ya pande zote mbili na nchi nyingine duniani.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, katika mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika jana, wakati akizungumzia sera ya kidiplomasia ya China na hali ya kisiasa na kiusalama duniani.

Wang Yi  pia  akizungumzia mahusiano kati ya China na Afrika amesema mwaka jana kwenye mkutano wa kilele wa kupambana na COVID-19 kati ya China na Afrika, Rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua mbalimbali za kusaidia nchi za Afrika.

“China inaendelea kuzisaidia nchi hizo, na hadi sasa China imetoa karibu shehena 120 za vifaa vya matibabu kwa Afrika, kutuma timu za wataalam wa afya na pia imetoa na inaendelea kutoa chanjo ya COVID-19 kwa nchi 35 za Afrika na kwa Kamati ya Umoja wa Afrika,” alisema.

Alisema hali ya jumla ya ushirikiano kati ya China na Afrika ni mzuri na kwamba huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na katika kipindi hicho thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka kwa mara 20.

Amesema uwekezaji wa China kwa Afrika umeongezeka mara 100, na idadi ya miji ya rafiki kati ya pande hizo mbili imefikia 150.

Alisema ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa mfano wa kuigwa kwenye ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Aidha, amekumbusha kuwa mwaka huu mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utafanyika nchini Senegal, na China inapenda kutumia fursa hiyo kuunga mkono Afrika kupata ushindi kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona, kuiunga mkono Afrika kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda, kuunga mkono mafungamano ya Umoja wa Afrika, na kuunga mkono masuala ya Afrika kutatuliwa kwa njia ya kisiasa barani Afrika.

Alisema ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na nchi za Afrika ni kujenga ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ lengo ni kuwa na jumuiya imara zaidi yenye hatma ya pamoja, hiyo itakuwa ni injini ya kudumu kwa Afrika kujiendeleza na kustawi.

“Ukanda mmoja, Njia moja” ni pendekezo lililoanzishwa na China mwaka 2013 kwa lengo la kuhimiza maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu duniani, hasa kwenye nchi zinazoendelea.

 

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi