loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kenya yatangaza masharti mapya kuingia nchini humo

KENYA imetangaza orodha ya nchi ambazo raia wake wakiingia nchini watatakiwa kukaa karantini ya siku 14, huku nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwa hazimo kwenye orodha hiyo.

Nchi hiyo imetangaza hatua hiyo katika kile inachoeleza kuwa ni sehemu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki za Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Burundi zimeorodheshwa katika nchi zaidi ya 200 ambazo wananchi wake hawatalazimika kukaa karantini.

Taarifa iliyotolewa jana na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Kenya (KCAA), ilibainisha kuwa, nchi sita za Brunei, Jamhuri ya Czech, Kuwait Hispania, Uswisi na Thailand wananchi wake waingiapo nchini humo watatakiwa kukaa karantine ya lazima.

“Abiria kutoka katika nchi hizo wanatakiwa kuwasilisha vyeti vinavyoonesha wamepima ugonjwa huo  ndani ya siku 72 kabla ya kuanza safari na kubainika kutokuwa na ugonjwa huku wakiwa hawana dalili zozote za mafua,” ilisema taarifa hiyo.

Raia wa nchi hizo pia watatakiwa kuonesha ushahidi wa maeneo watakayoishi kwa siku hizo 14 watakazokaa karantini kwa siku hizo 14.

Hii ni mara ya pili Kenya kuweka masharti kwa raia wa baadhi ya Kenya kuingia nchini humo tangu kuibuka kwa janga la corona.

Mara ya kwanza ilikuwa Agosti mwaka jana ilipozuia ndege kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania kutoingia nchini humo kwa kile ilichoeleza kukabiliana na ugonjwa wa covid-19 na baadaye Tanzania nayo ilizuia ndege za nchi hiyo kufanya safari Tanzania.

Hata hivyo, baada ya majadiliano baina ya pande hizo mbili ndege za pande zote ziliruhusiwa kuingia katika nchi hizo.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi