loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake Mtwara wajitoa kuboresha huduma za kinamama

WANAWAKE wajasiriamali wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wamechanga na kununua kitanda cha kujifungulia wanawake kwa ajili ya kusaidia Zahanati ya Likokona ambayo inapokea wanawake wanne mpaka sita kwa siku huku ikiwa na kitanda kimoja cha kujifungulia.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi kitanda hicho, Mganga Mfawidhi wa Zahana hiyo Rehema Akili amesema zahanati hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1974 inapokea wanawake zaidi ya 300 kwa mwaka huku wanawake wengine wakilazimika kujifungulia sakafuni.

Amesema kwa mwaka 2018 zahanati hiyo ilipokea wanawake 254 na kwa mwaka 2019 walipokea 229 na huku 2020 na wakipokea wanawake 330.
Amesema zahanati hiyo inahudumia vijiji 4 na kwamba ina watumishi 3 wakimo wauguzi wawili pekee.

Ameiomba serikali na wadau wengine kusaidia hiyo zahanati katika kuchangia vitanda na vifaa vingine ikiwemo ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama ambayo kwa sasa inajengwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

“Changamoto zetu kubwa ni idadi ndogo ya watumishi ambapo tuna watumishi watatu wakiwemo wauguzi wawili tu, uhaba wa majengo wa kutolea huduma,” alisema Akili.

Aliomba zahanati hiyo kusaidiwa katika kujenga jengo la wazazi kuboresha huduma za akina mama na kuongeza watumishi ili tuweze kutoa huduma bora kwa jamii yetu.

Pia aliomba serikali kuwajengea Kituo cha Afya kama walivyoahidi kwenye ilani ya CCM kuwa watawajengea kituo cha afya ili kuboresha huduma za afya.

Pia aliwashukuru akina mama hao kwa kuguswa kuchangia kitanda ambacho kwa sasa kitasaidia zahanati kupokea wanawake wanaojifungua.
Kwa upande wake, Mratibu wa kikundi cha akina mama wajasiriamali Eloisi Malisa amesema wanawake hao waliamua kuchangishana na kununua hicho kitanda ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

 


 

foto
Mwandishi: ANNE ROBI Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi