loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanesco yatoa vifaa vya milioni 6/- Shule ya ‘Kondoa Girls’

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani, wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wametoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni sita kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kondoa ‘ Kondoa Girls’.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUICO tawi la Tanesco, Prisca Maziwa alisema vifaa vilivyotolewa ni magadoro nane, mashuka na mito kwa ajili ya zahanati ya shule, sabuni na vifaa vya usafi, taulo za kike, vifaa vya michezo na vitabu vya masomo mbalimbali.

Aidha Afisa Mkuu Fedha wa Shirika hilo, Renatha Ndege aliwataka wanafunzi hao kuzingatia masomo yako kama wanataka kuwa super women.
Alisema, "Ili kufikia kuwa super women katika maisha yenu mzingatie Sana elimu, pia muwe na tabia njema, utii, utulivu, wasafi, mpendane na kubwa mumtegemee Mungu katika kila jambo."

Kwa upande wa Mkuu wa shule hiyo, Flora Nussu amewashukuru wanawake wa TANESCO kwa upendo wao kwa kuweza kuwachagua kushiriki nao katika siku ya wanawake na kuwaletea msaada wa vitu mbalimbali.

Naye Getrude Gadau, mwanafunzi wa shule hiyo aliwashukuru wanawake wa TANESCO kwa upendo wao na kuahidi kuutumia msaada waliopata vizuri na kuongeza juhudi katika masomo ya zaidi ya wanafunzi 600 wa shule hiyo.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi