loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mwinyi: Wakala wa Barabara wajitathmini

RAIS wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ameiagiza  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutoipa mradi wa ujenzi wa barabara kubwa Wakala wa Barabara visiwani humo kwa kuwa hawaiwezi kazi hiyo na badala yake wapewe kazi ya kuziba viraka.

Rais Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar alipokutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu ikiwa ni kikao cha kupokea ripoti ya maagizo aliyoyatoa alipowaapisha.

“Wakala wa barabara msifanye kazi ambazo hamziwezi ikiwemo ujenzi wa barabara na badala yake jikiteni katika kuziba viraka vya barabara, na barabara kubwa zote  zipewe kampuni kubwa zenye uwezo ambazo zitaweza kufanya kazi kwa ufanisi.”alisema Rais Mwinyi

Alisema wizara hiyo ina kazi kubwa ya kuhimarisha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, bandari pamoja na mawasilino hivyo ni vyema ikajitathmini.

Pia ameitaka Wizara hiyo ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, kuzihimarisha taasisi zake ipasavyo kwa kuwa wizara hiyo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar hivyo inapaswa kufanya juhudi za makusudi katika kuhakikisha inatekeelza vyema majukumu yake kutokana na taasisi zake kutegemewa kwa kiasi kikubwa katika kuhimarisha uchumi wa Zanzibar.

Aidha amesema haridhishwi na utendaji pamoja na ukusanyaji mapato katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume na kuitaka Wizara hiyo kuhakikisha inaweka miundombinu rafiki ya ukusanyaji wa kodi.

Kwa upande wa bandari, Rais Mwinyi amesema bado kuna uvujaji wa mapato kwa meli zinazotoa huduma za ndani na kuitaka wizara hiyo kulifanyia kazi suala hilo huku akisisitiza kuhakikisha fedha zote za serikali zinakusanywa kwa njia sahihi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi