MKUU wa Wilaya ya Arusha, Kenan Kihongosi amewataka watanzania kumuombea Rais John Magufuli kwa hali yoyote ile na kuepuka kebehi na kumdhalilisha kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza jana Jijini Arusha kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Kihongosi alisema amelazimika kusema hayo kutokana na matusi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii.
"Nimeshindwa kuvumilia imebidi niseme maana ukiangalia Twiter na kwenye mitandao mingine ya kijamii watu wanamkebehi na kumdhalilisha Rais wetu John Magufuli sasa unajiuliza kosa lake ni lipi au kuwajengea miundombinu mbalimbali au nini naomba tuache hii tabia mara moja,".
Alisema endapo watu wataendelea na tabia hiyo serikali haitawavumilia itashughulika nao.
Aidha alisema ni busara kwa wananchi wakajenga tabia ya kuheshimu viongozi wao.
"Ukimdhalilisha Rais unadhalilisha nchi yetu kweli hatutakubali… watu waache tabia hii inakera sana tunapaswa kumuombea ili aendelee kutuletea miradi mingine,"alisema huku akishangiliwa na madiwani wa baraza hilo..
Pia alitoa rai kwa madiwani wa Jiji hilo kuhakikisha wanashirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
2 Comments
Emmanuel Mallya
Nawapongeza sana..
Hubert remigius
Leaders should be respected for sure.