Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kuwa miradi iliyo ndani ya ilani ya uchaguzi na ambayo Rais John Pombe Magufuli alipita na kutoa ahadi, itatekelezwa.
Amesema hayo leo wakati akiongea na wananchi katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, katika ziara ya kikazi mkoani humo, na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha huduma zinapatikana kila kona ya Tanzania ikiwa ni pamoja na maji safi na salama, huduma za afya bora na elimu katika ngazi zote ikiwemo misingi, sekondari na vyuo.
Makamu wa Rais leo ameanza ziara ya siku sita mkoani Tanga kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi.