loader
Dstv Habarileo  Mobile
MAGUNOMICS:  Uchumi ulivyojielekeza  katika miradi ya kimkakati

MAGUNOMICS: Uchumi ulivyojielekeza katika miradi ya kimkakati

TUNAINGIA siku nyingine ya mwendeklezo wa makala hii inayoangalia sera za mageuzi ya kiuchumi zilizotekelezwa na Dk Joh Magufuli (JPM) kiasi cha kuiharakisha Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati katika kipindi kifupi na kuishangaza dunia.

Katika makala haya tumeziita sera hizi ‘Magunomics’  kwa maana ya Magu (Magufuli) na nomics (economics-uchumi) yaani uchumi uliotekelezwa na JPM.

Baada ya kuangalia Magunomics kwa upande wa sera za kibajeti, uongezaji mapato na dhana ya kuwajali wanyonge, wiki jana tuliangalia namna serikali yake ilivyojizatiti katika kukusanya kodi na kuhakikisha nchi inanufaika na raslimali zake na kudhibiti matumizi ya serikali.

Leo tunaangalia ni maeneo gani pesa zilizookolewa zilipelekwa na serikali ya Magufuli. Kimsingi, pesa zilizokuwa zinaokolewa zilipelekwa kwenye sekta muhimu za kimkakati

Ongezeko la makusanyo na fedha zilizookolewa kutoka kwenye matumizi mbambali yaliyokuwa hayana tija baadhi yakiwa ya hovyo, yaliiwezesha serikali kutekeleza miradi muhimu ya kimkakati kama ifuatavyo:

Afya

Taifa la watu wenye afya maana yake ni kuongeza tija katika kazi kwani inaokoa muda ambao watu hupoteza kwa kuugua badala ya kuzalisha au kuuguza. 

Bajeti ya dawa na vifaa tiba iliongezeka kutoka Sh bilioni 31 mwaka 2015 mpakazaidi ya Sh bilioni 260.  Mwaka 2016 Serikali ilitenga Sh bilioni 251 kwa ajili ya dawa na vifaa tiba na yote ilitolewa.

Kwa miaka mitatu tu ya kwanza ya utawala wake, vituo 268 vya afya vilikuwa vineshajengwa nchini kote.

Ununuzi wa kifaa cha CT-Scan kipya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kiliwezesha kutoa hudumia kwa wagonjwa 50 kutoka 20 kwa siku.

Matibabu mengi ya kibingwa kama vile kuboresha na kubadilisha figo, matatizo ya moyo, matizo ya kibyongo (scoliosis), mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu na mengineyo ambayo zamani yalilazimu Watanzania kuyafuata nje ya nchi sasa yanafanyika hapa nchini.

Ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ya afya, serikali ya Awamu ya Tano ilihamasisha wananchi wajiunge na bima ya afya na mifuko ya hafadhi ya jamii na ilikuwa inaandaa mpango wa kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na bima.

Elimu bila malipo

Mwalimu Nyerere alipata kusema kwamba ukitaka kumsaidia mtoto wa maskini mpe elimu na nchi takribani zote zinazofanya vizuri zimewekeza vya kutosha kwenye elimu.

Utekelezaji wa kutoa elimu bure umeendelea kuwanufaisha wanafunzi wa elimu ya awali hadi sekondari nchini kote na kusaabisha ongezeko kubwa la wanafunzi shuleni.

Kwa shule za msingi, serikali inatoa Sh bilioni 20 kwa mwezi kugharamia ada, posho za wakuu wa shule, uendeshaji wa shule na chakula kwa bweni na Sh bilioni 3 kwa ajili ya kugharamia mitihani ya darasa la nne, saba, kidato cha II na cha nne IV.

Kwa mantiki hiyo, jumla ya Sh bilioni 23 zinatolewa kwa mwaka kugharimia elimu bure. Matokeo yake, uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka wanafunzi milioni moja hadi zaidi ya milioni mbili.

Kwa upande wa sekondari, wanafunzi waliokuwa wameandikishwa walikuwa 483,072. Vilevile, shule kongwe 89 zilikarabatiwa upya kila shule ikitengewa kati ya Sh milioni 800 hadi shilingi bilioni moja kulingana na aina ya ukarabati.

Halikadhalika ujenzi wa maabara katika shule zote na ununuzi wa vifaa vya maabara ulifanyika.

Serikali pia imekuwa ikigharamia wanafunzi wenye uhitaji wa elimu ya juu kwa ada, matumizi na vifaa kwa jumla ya Sh bilioni 483 na hivyo idadi ya wanaopata mikopo kuongezeka kutoka 98,000 mpaka zaidi ya 121,000.

Miradi ya maji

Kuna miradi mingi ya maji ambayo imejengwa na inaendelea kujengwa nchini kote. Miradi mikubwa ni pamoja na mradi wa bilioni 550 kutoka Ziwa Victoria kwenda mikoa ya Tabora na mikao ya jirani.

Kwa Arusha kulikuwa na mradi wa Sh bilioni 476 na mradi wa maji katika miji 17 na Zanzibar kwa gharajma ya shilingi trilioni 1.2.

Maeneo mengi nchini ambayo hayajawahi kupata maji ya bomba toka kuumbwa kwa ulimwengu, yalipata maji safi na salama katika kipindi kifupi cha utawala wa JPM.

Yapo maeneo katika jiji la Dar es Salaam, kama vile Kimara ambayo wananchi walikuwa wanalazimika kununua maji kwenye maboza kati ya Sh 150,000 hadi 200,000 kwa mwezi lakini sasa baada ya kuwekewa mabomba wanalipa bili kati ya Sh 15,000 na 25,000 tu kwa mwezi.

Wananchi wengi wameunganishiwa maji na kutakiwa kulipia gharama kidogo kidogo kwa miezi sita hadi mwaka na wenye madeni kulipia kidogo kidogo badala ya kukatiwa maji na hatimaye shirika kukosa wanachodai.

Ujenzi wa barabara

Katika kipindi kifupi serikali ilijenga zaidi ya kilometa 1,500 za barabara kwa fedha za ndani na pia ikajenga madaraka mtambuko ya Tazara na Ubungo katika jiji la Dar es Salaam. Kukamilika kwa madaraja hayo mtambuko kumepunguza foleni iliyokuwa kero kubwa kwenye maeneo hayo.

Mengine yaliyokuwa yanafanywa na serikali ya JPM ni upanuzi wa barabara ya Ubungo-Chalinze, ujenzi wa daraja la Coco Beach linalopita juu ya bahari kutoka barabara ya Barack Obama hadi Masaki na daraja la Busisi-Kigongo ni miradi muhimu ambayo kukamilika kwake kutachochea sana uchumi wa Tanzania.                              

Ujenzi reli ya kisasa

Serikali ya JPM ilikuwa inaendelea na ujenzi wa reli ya kisasa yenye kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway - SGR) kutoka Dar es Salaam-Tabora-Kigoma, Tabora-Mwanza na Tabora-Mpanda.

Baadaye, ujenzi utaendelea hadi nchi za Rwanda, Burundi na DR Congo. Kipande cha Dar es Salaamu mpaka Dodoma pekee kilitazamiw akugharimu Sh trilioni 7.1 na ujenzi wa reli hiyo katika ya Dar Morogoro uko katijka hatua za mwisho.

Serikali pia ilisshughulikia utengenezaji wa mabehewa 1,590 ya kusafirisha mizigo na abiria, vichwa 25 pamoja na mitambo.

Treni ya kisasa itakuwa ikisafiri kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa na ile ya mizigo itasafiri kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa.

Ujenzi wa reli hiyo utakapokamilika utaharakisha usafiri wa mizigo na abiria kwa gharama nafuu, utachochea utalii wa ndani, biashara na uwekezaji na uzalishaji wa mazao ya kilimo.

 

*Itaendelea kesho...

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2cdfcb2c7a596ba6f97fdf290f52ccd4.jpg

HISA milioni 15 zenye thamani ya shilingi ...

foto
Mwandishi: Profesa Kitojo Wetengere

1 Comments

  • avatar
    Emmanuel gakuba
    18/05/2021

    wasalaam wasomaji wa gazeti la mtandaoni habari leo; ni msomaji ni kiwa na jina la bwanyenye mkwasi, naafiki mawazo na maoni ya kufufua uchumi wa watanzania ikiwemo ujenzi wa muundo mbinu, elimu,afya ya jamii na mengineyo . swala bwanyenye mkwasi ni hili niombeeni waheshimiwa mawaziri &wakuu wa mikoa yenye mradi wangu kwani umevuma mabara yote duniani. kipengere wahedi **1 kwanini bwanyenye mkwasi anaombaomba kigali wakati mapesa ya meli yalitumwa kwenye benki zao **2kwanini hatutibiwi maradhi yetu kwenye senotarium LAKE GENEVA wakati tumenunuliwa**3kwa nini tusisafirishwe kwenda uswiss kama mjasiriamali wa Tanzania kwani Marekani na kwinginepo mrituwakilisha**mwisho tutumieni ndege yetu uwanja wa mataifa Kanombe tumahututi** aksanteni hategemea mafanikio mema kwenu. ndimi ; Bwana EMMANUEL GAKUBA M BWANYENYE MKWASI** MUHIMA **HOTEL OKAPI STREET// NYARUGENGE// RWANDA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi