loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mongella kuzindua Michezo ya Mei Mosi

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Michezo ya Mei Mosi utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mwaka huu, imeelezwa.

Katibu wa Kamati ya Mei Mosi Taifa, Mosi Makuka alisema Dar es Salaam jana kuwa michezo hiyo ya Mei Mosi itaanza Aprili 16, lakini uzinduzi wake rasmi utafanyika Aprili 18, 2021 kwenye uwanja huo huo.

Alisema kuwa hadi sasa mbali na Mambo ya Nje, timu zingine zilizokwisha thibitisha kushiriki ni pamoja na Uchukuzi, Tanesco, Tanapa, TRA na Ukaguzi.

Makuka alizitaka timu zingine kuthibitisha kushiriki haraka ikiwa pamoja na kuorodhesha michezo watakayoshiriki ili waandaaji waweze kuandaa viwanja vya kuchezea michezo hiyo.

Alisema kuwa michezo ya mwaka huu inatarajia kumazika Aprili 30, ambapo alizitaka timu zilizotwaa ubingwa katika micheao ya mwaka juzi, kurejesha vikombe haraka ili vishindaniwe mwaka huu.

“Timu zote zilizotwaa vikombe katika michezo ya mwaka juzi wavirudishe mapema ili viweze kushindaniwa mwaka huu, “alisisitiza Makuka.

Alisema kuwa wengine bado wamethibitisha kwa mdomo kushiriki, lakini wanatakiwa kuwasilisha uthibitisho huo kwa maandishi ikiwa pomoja na kueleza michezo watakayoshiriki.

Alitaja michezo itakayochezwa mwaka huu kuwa ni pamoja na soka, mbio za baiskeli, netiboli, karata, drafti, kuvuta kamba na bao.

Aliwataka waajiri kutoa ruhusa kwa wafanyakazi wao, kwani mashindano hayo yana umuhimu mkubwa , ambapo mbali na kuimarisha afya pia yanawawezesha wafanyakazi wa taasisi mbalimbali kufahamiana na kurahisisha utendaji kazi.

Alitoa wito kwa timu  kuendelea na mazoezi ili kujiandaa kwa mashindano hayo, ambapo washindi wake watakabidhiwa vikombe wakati wa kileleni cha Mei Mosi.

 

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi