loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Atenguliwa ndani ya Saa 11 baada ya Rais kumteua

RAIS Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Thobias Richard ikiwa ni ndani ya saa 11 tangu kuteuliwa kwake.

Jana April 4, 2021 saa nne usiku, Rais Samia alimteua Thobias Richard kuwa miongoni mwa wakuu wa mashirika aliowateua lakini leo asubuhi ametengua uteuzi huo na kumrejesha Dk James Mataragio kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.

Dk Mataragio ndiye alikuwa Mkurugenzi wa shirika hilo kabla ya uteuzi wa Richard na kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, Dk Mataragio anaendelea na majukumu yake mara moja.

Aidha taarifa hiyo iliyotolewa leo asubuhi Aprili 5, 2021 inaeleza kuwa uapisho wa viongozi walioteuliwa jana utafanyika kesho Aprili 6, saa 4 kamili asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi