loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Filamu ya Binti kuonyeshwa leo nchi nzima

FILAMU ya Binti ambayo imegusa changamoto mbalimbali za kimaisha zinazowakuta wanawake kwenye nyanja za mahusiano, uchumi, afya na masuala mengie mbalimbali itaoneshwa leo katika kumbi zote za sinema mjini.

Filamu iliyoandaliwa kwa mwaka mzima na Seko Shamte pamoja na ndugu wawili, Angela Ruhinda na Alinda Ruhinda wa kampuni ya Black Unicorn Studio.

Binti imehakisi maisha hali wanayopitia wanawake huku ikihusisha zaidi mazingira ya Mbezi, Temeke, Sinza, Masaki, Oysterbay, Upanga na Mikocheni yote ni maeneo ya Dar es Salaam.

Akizungumzia zaidi filamu hiyo, Seko alisema imekidhi vigezo vya kuoneshwa kwenye kumbi za filamu kutokana na ubora,imechaguliwa kushiriki kwenye Tamasha la Filamu la PAN nchini Marekani.

Kwa upande wake Angela Ruhinda alibainisha kuwa, Tanzania inaweza kuwa na filamu bora zaidi zitakazowezesha kushiriki kwenye tuzo za filamu za kimataifa.

Alisema,”Binti imeonesha uwezo wa watanzania kuigiza na hata uwezo wa kutayarisha filamu za kisasa zenye hadhi ya kimataifa, hakika kazi ndiyo kwanza inaanza na tutegemee makubwa zaidi.”

Mwanamitindo mahiri wa kitanzania anayefanya kazi nchini Marekani, Millen Magese akiizungumzia filamu hiyo anasema kuwa ni hatua nzuri kuelekea kwenye uboreshaji wa filamu za Tanzania huku akiisifia kwa namna ambayo imekuwa ya kisasa. 

Naye Mwanamitindo Flaviana Matata alisema filamu ya Binti imekidhi viwango vya kimataifa na kuwa ni wakati kwa watanzania kuwekeza kwenye filamu za aina hiyo zenye ubora, ujumbe zinazoweza kuoneshwa kwenye majumba ya sinema ndani na nje ya nchi.

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi