loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge: Wanawake kopeni mfanye biashara

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Dk Christine Ishengoma, ameshauri wanawake kukopa katika taasisi za fedha zikiwamo benki ili waanzishe na kuendeleza biashara.

Aliyasema hayo katika kongamano la wanawake lililoandaliwa na Benki ya CRDB mjini Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake kuhusu namna ya kufanya biashara.

Aliwahimiza wanawake kutoogopa kukopa fedha benki na akawakumbusha wajibu wa kurejesha kwa wakati mikopo wanayoichukua huku wakizingatia kutumia mikopo hiyo kwa malengo kusudiwa.

Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Huduma za Kibenki CRDB, Recho Senni, alisema benki hiyo imeboresha huduma za kifedha kwa wanamke ili wajikwamue kiuchumi kwa kutoa mkopo ya riba nafuu.

Alitaja changamoto wanazokumbana nazo wanawake wanapochukua mikopo kutoka kwa wakopeshaji wasio rasmi kuwa ni pamoja na riba kubwa zinazowafanya wanawake wengi kushindwa kufikia malengo yake.

Meneja wa Biashara Kanda ya Kati wa Benki ya CRDB, Jane Maganga, alisema benki hiyo imejipanga kuwasaidia wanawake kwa kubuni njia mbalimbali.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi