loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Marekani yarudi tena mazungumzo ya nyuklia

MAREKANI imejiunga kwenye mazungumzo yanayolenga kufufua makubaliano ya nyuklia na Iran yanayofanyika Vienna, Austria, ambayo serikali ya Rais wa zamani wa nchi hiyo,  Donald Trump ilijiondoa mwaka 2018.

Nchi sita zinashiriki mazungumzo hayo kutafuta njia za kuhakikisha kuwa Marekani chini ya Rais Joe Biden inaondoa vikwazo vilivyowekwa na mtangulizi wake dhidi ya Iran ili iweze kutekeleza masharti ya programu ya nyuklia.

Maofisa wa kidiplomasia kutoka Uingereza, Ufaransa Ujerumani, Urusi na China wanahudhuria mazungumzo hayo, ambapo Iran imetoa sharti la kuondolewa vikwazo vyote ili iweze kukaa meza moja na Marekani.

Balozi wa Urusi katika mashirika ya kimataifa mjini Vienna, Mikhail Ulyanov, alisema mazungumzo yaliyofanyika Jumanne iliyopita yalikuwa na mafanikio, huku makundi mawili ya wataalamu yanayoshughulikia masuala ya vikwazo na masuala ya nyuklia wakipewa jukumu la kutambua hatua madhubuti za kusonga mbele katika mazungumzo hayo.

Ulyanov alisema wataalamu wameanza kazi yao ili kufanikisha suala hilo ambalo haitakuwa rahisi kwani kurejeshwa tena kwa makubaliano hayo hakutakuwa kwa haraka.

"Itachukua muda, kwa kiasi gani? Hakuna anayejua. Jambo la maana ni kuwa kazi ya kufikia malengo hayo imeshaanza,'' alisema mwanadiplomasia huyo wa Urusi anayefanya shughuli zake mjini Vienna.

Awali, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Ned Price alitoa tahadhari kabla ya mkutano huo akiwaambia waandishi wa habari jijini Washington kuwa:  ''Hatutarajii mafanikio ya mapema na haraka, kwani tunatatarajia mazungumzo kuwa magumu.''

Mjumbe Maalumu wa Marekani nchini Iran, Robert Malley alisema wiki iliyopita kuwa, lengo lilikuwa ni kutafuta makubaliano ya pande zote pamoja na washirika wengine wa Ulaya na Asia.

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: VIENNA, Austria

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi