loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Netanyahu ateuliwa kuunda serikali Israel

RAIS wa Israel, Reuvin Rivlin amempa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu kazi ngumu ya kujaribu kuunda serikali ingawa hakupata viti vya kutosha bungeni kuunda serikali.

Katika tangazo lake jana, Rais Rivlin alikiri kuwa hakuna kiongozi wa chama chochote aliye na uungwaji mkono unaohitajika ili kuunda serikali ya muungano katika Bunge la Israel lenye viti 120.

Baada ya kushauriana na vyama 13 ndani ya Bunge lililochaguliwa upya, Rivlin alisema Netanyahu ana nafasi nzuri kuliko mgombea mwingine yeyote ya kuunda serikali mpya.

Bunge la Israel lina viti 120 hivyo mshindi atakayeunda serikali bila kuungana na chama kingine anatakiwa kupata viti 60 ikiwa ni asilimia 50 ya viti vyote bungeni.

Pamoja na kupata ushindi mwembamba katika uchaguzi wa wiki iliyopita, haitakuwa rahisi kwa Benjamin Netanyahu kuunda serikali kutokana na kuzongwa na tuhuma za rushwa na maandamano ya umma ya kumtaka ajiuzulu.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: TEL AVIV, Israel

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi