loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ligi Kuu kurejea leo Na Martin Mazugwa

LIGI Kuu ya Tanzania Bara  inaendelea leo kwa viwanja viwili kuwaka moto wakati mechi zitakapoendelea baada ya kusimama kwa siku 21 kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.

Magufili alifariki dunia Machi 17 na kuzikwa nyumbani kwake Chato Machi 26, mwaka huu.

Katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Mbeya City itawaalika Kagera Sugar kutoka Bukoba, huku Namungo ikiwakaribisha Ihefu FC katika Uwanja wa Majaliwa, Ilulu, Lindi.

Mbeya City itaingia katika mchezo huo ikiwa katika nafasi ya 16 katika timu 18 zinazoshiriki ligi hiyo, huku wapinzani wao Kagera wakiwa nafasi ya 13, wakati Namungo wakiwakaribisha Ihefu wakiwa na maumivu baada ya kupoteza mchezo wa Shirikisho Afrika dhidi ya Nkana ya Zambia.

Akizungumza na HabariLEO jana, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Mathias Lule alisema hivi sasa wanachotafuta ni pointi tatu katika kila mchezo ili kujitoa katika eneo la kushuka daraja.

“Tupo katika nafasi mbaya, kitakacho tutoa hapa ni ushindi pekee, naamini vijana wangu wataenda kufanya kile tulichofanyia kazi mazoezini,” alisema Lule.

Naye Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza alisema ana amini utakuwa mchezo mgumu kutokana na kila timu kusaka alama tatu lakini vijana wake wapo tayari kwa ajili ya mapambano.

“Huu ni mchezo wangu wa kwanza nikiwa hapa lakini naamini vijana wangu hawataniangusha, lengo letu ni kuwa katika nafasi 10 za juu,” alisema Baraza.

Kocha Mkuu wa Namungo FC, Hemed Suleiman ‘Morocco’ alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kwamba ameyafanyia kazi mapungufu ya kikosi chake hivyo ana amini vijana wake hawatamuangusha.

“Hatujapata matokeo mazuri katika mchezo uliopita, lakini tumesahau ya nyuma tunasonga mbele lengo letu ni kushinda kila mchezo ulio mbele yetu,” alisema Suleiman.

Naye Kocha Mkuu wa Ihefu, Zeberi Katwila alisema anajua ana kazi kubwa ya kuitoa timu katika nafasi iliyopo hivi sasa na kwamba malengo yao ni kubaki katika Ligi Kuu Tanzania Bara hivyo wamejipanga kufanya vizuri katika kila mchezo ulio mbele yao.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi