loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuchel: Moto wa Mount “Hapana”

Baada ya kiungo Mason Mount kutundika msumari mmoja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FC Porto mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amesifu kiwango cha nyota huyo na kwamba amekuwa bora katika michezo ya hivi karibuni.

Mount alikuwa wa kwanza kufunga bao hilo dakika ya 32, kabla ya beki Ben Chilwell kukamilisha idadi ya mabao hayo ya ugenini katika mchezo wa raundi ya kwanza wa michuano hiyo uliopigwa dimba la Ramon Sanchez Pizjuan Sevilla.

Kiungo huyo wa zamani wa Derby Country amefunga mabao matatu katika michezo minne ya mwisho. “Bao lilikuwa la kiufundi na matumizi ya akili,”amesema Tuchel

Michezo yote miwili inafanyika Hispani katika Uwanja wa Sevilla kutokana na vizuizi vya maambukizi ya virusi vya corona vilivyowekwa kati ya Ureno na Uingereza hii inamaana kwamba mchezo wa jana Porto alikuwa nyumbani na mchezo ujao Chelsea atakuwa mwenyeji

 Tangu Tuchel alipojiunga na Chelsea mwezi Januari, Mount amefunga mabao mengi (5) kuliko mchezaji yoyote wa timu hiyo.

THOMAS Tuchel amesema Chelsea inakwenda fainali ...

foto
Mwandishi: SEVILLA, Spain

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi