loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbappe kumbe aliwatamani Bayern

Kylian Mbappe ametupia kambani mabao mawili yaliyoiweka PSG katika mazingira mazuri ya kutinga nusu fainali, baada ya kuwafunga Bayern Munchen mabao 3-2 mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Allianz Arena.

Mchezo huo uliokuwa na ufundi wa aina yake, ulikutanisha mafahali wawili ambao msimu uliopita walikutana hatua ya fainali ya michuano hiyo ambapo Bayern waliondoka kifua mbele kwa kutwaa ubingwa huo.

Beki raia wa Brazil, Marquinhos alifunga bao lake dakika ya 28 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Angel Di Maria na kufufua matumaini mengine ya kuingia katika hatua ya nusu fainali.

Baada ya kufunga mabao hayo , Mbappe sasa amefunga mabao manane katika michuano hiyo akiungana na mfaransa Wissam Ben Yedder aliyefanya hivyo msimu wa  2017-18 na David Trezeguet msimu 2001-02.

Mabao hayo yanakuja baada ya wiki kadhaa zilizopita kufunga mabao matatu ‘hat-trick dhidi ya Barcelona.” Kama nilivyosema napenda aina hii ya mchezo,”alisema Mbappe baada ya mchezo huo.

“Siku zote walikuwa haendi katika mstari ninaoutaka nap engine hawawezi kwa siku za usoni, ila siko hapa kujificha napenda aina hii ya mchezo,”aliongeza.

THOMAS Tuchel amesema Chelsea inakwenda fainali ...

foto
Mwandishi: MUNICH, Ujerumani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi