MDHIBITI na Mkaguzi wa Hesabu za serikali CAG, Charles Kichere amesema deni la taifa limepanda kwa asilimia saba.
Kichere ameyasema hayo leo jijini Dodoma ambapo alisema matokeo ya ripoti yake yamebaini kuwa mwenendo wa deni la taifa hadi kufikia Juni mwaka 2020, lilikuwa shilingi trilioni 56.76.
Amesema kati ya fedha hizo, deni la ndani ni shilingi triliolini 15.52, deni la nje ni trilioni 41.24 hivyo kufanya kuwa na ongezeko la deni trilioni 3.65 sawa na asilimia saba ukilinganisha na deni la shilingi trilioni 53.11 lililoripotiwa 2018/2019,”
CAG Kichere amesema ongezeko la deni la sasa hivi linajumlisha bilioni 652 la deni la ndani na shilingi trilioni tatu za deni la nje.
“Deni hili linahimilika kwa mujibu wa vigezo ,lakini limekuwa likiongezeka kila mwaka.” alisema