MDHIBITI na Mkaguzi wa Hesabu za serikali (CAG), amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikusanya mapato chini ya kiwango kilichokadiriwa.
CAG ameyasema hayo leo jijini Dodoma na kudai kuwa TRA ilikusanya shilingi trilioni 17.92 ikiwa chini ya makisio ambayo ilikadiriwa kukusanya shilingi trilioni 19.45.
Amesema kutokana na hali hiyo kuna upungufu wa shilingi trilioni 1.49 sawa na asilimia nane.
“Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikusanya shilingi trilioni 17.92 ikiwa chini ya makisio ambayo ilikadiriwa kukusanya shilingi trilioni 19.45 na hivyo kuwa na upungufu wa shilingi trilioni 1.49 sawa na asilimia nane. “ alisema CAG Charles Kichere
Alisema TRA ilikuwa na changamoto mbali mbali ya ukusanyaji mapato ya bidhaa zinazopita kwenda nje zenye ushuru wa forodha shilingi bilioni 5.14 lakini hazikuthibitishwa kutoka nchini, pia kulikua na mafuta yaliyopita muda wa matumizi yaliyokuwa yanaenda nje yenye thamani ya shilingi bilioni 12.14 hazikukusanywa