loader
Dstv Habarileo  Mobile
Jamii ishiriki kuwezesha watoto wenye usonji kujitegemea ukubwani

Jamii ishiriki kuwezesha watoto wenye usonji kujitegemea ukubwani

WADAU mbalimbali kupitia taasisi na mashirika yao wamekuwa wakizungumza namna bora na sahihi za kuhakikisha watoto wenye tatizo la usonji (autism) wanatambulika kwenye jamii na kuwezeshwa kuishi kama watu wengine.

Jana, hapa nchini wadau hao ikiwamo Serikali, wamekutana tena kuzungumzia changamoto zinazowakuta watoto wenye tatizo hilo na namna bora zaidi ya kuwawezesha kuishi baadae wakiwa vijana na watu wazima wenye usonji wanaoweza kujitegemea.

Ni katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Usonji Duniani ambayo kwa kawaida hufanyika Aprili 2 kila mwaka lakini kutokana na msiba wa kitaifa wa hayati Dk John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania, walisogeza mbele na kuifanya jana, wadau walikubaliana kuanzia ngazi ya familia, kijiji na mtaa kuwatafuta watoto hao na kujenga mfumo endelevu.

Mfumo huo ndio hasa utakaowezesha kuwafuatilia kuanzia wanapozaliwa, ukuaji wao kipindi cha utoto, ujana na utu uzima ili kuwawezesha kupata elimu na ujuzi hadi ngazi ya vyuo, kusaidia kupunguza gharama za matibabu yao na kuwawezesha kutoa mchango katika jamii kupitia vipawa walivyonavyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Godwin Mollel akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, alikiri kuwa Serikali haihitaji utafiti

kuhusu watoto au tatizo hilo kwa kuwa lipo na watoto wapo bali kinachohitajika ni kuungana na wadau wa sekta binafsi, kuweka mfumo wa kuwatafuta wote na kuwawezesha kupata elimu na ujuzi maishani.

Binafsi naungana na wadau hao akiwamo Naibu Waziri, Dk Mollel, kuikumbusha jamii kwamba, tatizo la usonji ambalo kwa hapa nchini takwimu za mwaka 2018 zinaonesha kuna wanafunzi 1,416 waliosahiliwa shuleni wenye tatizo hilo, si kazi ya Serikali na familia zenye watoto au watu wenye tatizo hili, bali ni la wote hasa ikizingatiwa kuwa, watoto wanaozaliwa na usonji wana vipaji na uwezo mkubwa.

Tukiweka nguvu ya pamoja katika kutafuta namna ya kutambua vipaji walivyo navyo na kuwepo na nafasi katika vyuo kwa mfano vya Ufundi (Veta) na vinginevyo kuwawezesha kupata elimu ya ufundi baada ya kumaliza elimu ya msingi au sekondari ambayo nako hupata elimu maalumu, wataweza kutumia ujuzi wao kujipatia kipato na kuishi wakiwa na tatizo hilo lakini wakijitegemea.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/eb7acdea2491b7390c706cafada33430.jpeg

LEO katika mwendelezo wa makala za ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi